Michezo

Man City Ubingwa EPL huooo

0
Man City Ubingwa EPL
Manchester City

Timu ya Manchester City, inakaribia kutwaa ubingwa EPL baada ya kuichapa Everton mabao 3-1 juzi katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza uliochezwa katika Uwanja wa Goodison Park, London.

Manchester City inatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu kama ikifanikiwa kuifunga Manchester United katika mchezo utakaochezwa wiki hii.

Mchezo huo unatarajiwa kuridima Uwanja wa Etihad, ambapo kama Man City wakiibuka na ushindi watajihakikishia ubingwa msimu huu 2017/2018.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alisema kwamba baada ya kupata ushindi huo, wanajipanga kutwaa ubingwa msimu hii.

Alisema ana kikosi imara kwajili ya kushinda mchezo unaofuata na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

“Tumepata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Everton na sasa tunajipanga kucheza mchezo mwingine dhidi ya Manchester United ambao ni mchezo muhimu kwetu,” alisema Guardiola.

Soma pia:  Klopp: Liver haitatumia fedha nyingi kusajili

Katika msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza, Man City ina point 84 inafuatiwa na Manchester United yenye alama 68 wakati Liverpool ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 66.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo