Michezo

Mambo yaiva Simba vs Al Ahly Taifa kesho

0
Simba vs Al Ahly
Simba SC

Wapinzani wa Simba SC, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wanatarajiwa kutua nchini leo tayari kwa mchezo wao wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa kundi D na Simba ina kazi ngumu ya kubadili matokeo baada ya kufungwa mabao 5-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Misri mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentus Magori alisema, taarifa za awali walizozipata kutoka kwa Waarabu hao ni kuwa watafika nchini leo wakiwa na msafara wao kamili.

Alisema kuwa kocha wao Patrick Aussems anaendelea na maandalizi ya kuiandaa timu ili kupata pointi tatu ambazo wanazihitaji kwa udi na uvumba.

Soma pia:  Simba, Azam macho yote CECAFA Kagame

“Wametupa taarifa kuwa wanakuja kesho (jana) na ndege ya Egypt Air kwa mimi sijajua ni mda gani hasa watakuwa wameshafika, tumejipanga kuwapokea kwa taratibu zote zinazotakiwa… “Tupo tayari kwa mchezo huo kama tulivyokwisha kuzungumza, maandalizi bado yanaendelea chini ya kocha, tunajua ushindi huwa hautafutwi nje ya uwanja ila unapatikana ndani kwa hiyo maandalizi yote yanalenga kuifanya timu iweze kupambana siku ya mchezo,” alisema Magori.

Al Ahly wanakuja nchini ikiwa ni baada ya siku moja kumaliza mchezo wao wa Ligi Kuu Misri dhidi ya Haras El Hodood ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Hamdi Fathi dakika ya 45.

Katika mchezo huo kocha wa Ahly Martin Arrospide alitumia mbinu kama aliyoitumia Aussems katika mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC ambapo Simba ilishinda mabao 3-0.

Soma pia:  Mtibwa Sugar: Sasa ni zamu ya Simba

Arrospide aliamua kuwapumzisha wachezaji wake wanne walioanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo uliopita ambao ni Mohammed Hany, Amir Al Sulaya, Hesham Mohammed na Karim Nedved, kama alivyofanya Aussems dhidi ya Mwadui alipowapumzisha Emmanuel Okwi, Jonas Mkude Jjuko Murshid, Asante Kwasi na Nicolas Gyan.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo