Michezo

Lewandowski na Coman wamezichapa wakiwa mazoezini Bayern

0
Lewandowski na Coman wamezichapa
Robert Lewandowski na Kingsley Coman

Mshambuliaji mkongwe wa Bayern Munich, Robert Lewandowski na winga wake Kingsley Coman, wamezichapa ‘kavukavu’ wakiwa mazoezini, kocha wa miamba hiyo ya soka la Ujerumani Niko Kovac, amethibitisha.

Kocha huyo raia wa Croatia, ambaye pia ni nyota wa zamani wa Bayern Munich, amesema wakali wake hao wataadhibiwa kutokana na kitendo chao hicho walichofanya mazoezini Alhamis, kabla ya jana Ijumaa kujifua pamoja.

Wakali hao walikwaruzana katika mazoezi ya Bayern, wakati wakijiandaa kwa pambano la Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ dhidi Fortuna Dusseldorf.

“Watatu kati yetu tumeshazungumza juu ya hilo. Wachezaji wote wameomba radhi kutokana na kitendo cha ukosefu wa nidhamu walichoonyesha,” alisema Kovac na kuongeza: “Watawajibishwa, ingawa hakutakuwa na adhabu ya fedha. ”Lewandowski ni kinara wa mabao katika Bundesliga alikofumania nyavu mara 21 akiwa pia anaongoza kwa mabao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), alikofunga mabao nane, ingawa timu yake imetupwa nje hatua ya 16 Bora na Liverpool.

Soma pia:  Ujerumani warudi nyumbani vichwa chini

Comments

Comments are closed.

More in Michezo