Michezo

Kukosa nidhamu kwaitoa Senegal Kombe la Dunia

0
Kukosa nidhamu kwaitoa Senegal Kombe la Dunia
Timu ya taifa ya Senegal

Kutokuwa na nidhamu kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal kumewafanya waiage michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Russia.

Simba wa Teranga wametolewa kwenye hatua ya makundi baada ya kuwa na kadi nyingi za njano na kuizidi timu ya Japan, ambayo walikuwa wakishindania nafasi hiyo ya pili ya Kundi H kufuzu hatua ya 16 bora.

Timu hiyo ambayo ndiyo ilikuwa tumaini pekee kwa  bara la Afrika baada ya kuanza vyema mashindano hayo, ilitolewa baada ya kutandikwa bao 1-0 dhidi ya  Colombia.

Katika kundi hilo, Senegal na Japan zina pinti na mabao sawa ya kufungwa na kufunga ambayo ni manne kwa kila timu, lakini wawakilishi hao wa Afrika wametolewa kwa sababu ya uchezaji usio na nidhamu.

Soma pia:  Ufaransa, Denmark zafuzu 16 bora Kombe la Dunia

Japan imefuzu kutokana na rekodi ya nidhamu kwa wachezaji wake ilionysha ambapo katika mashindano hayo walionyeshwa kadin nne za njano pekee huku Senegal wakilimwa kadi sitta za njano.

Ingawa Japan ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Poland ambao tayari wameaga machindano hayo kutokana na kuwa na pointi tatu, lakini haikutosha kuizuia Japan kupenya.

Kutoka kwa Senegal kunahitimisha safari ya nchi tano za Afrika kuishia hatua ya makundi ikifuata Misri, Morocco, Tunisia, na Nigeria ambazo tayari zimeshaaga.

Kutoka kwa Senegal hakupishani sana na ilivyofungwa Nigeria kwenye mechi dhidi ya Argentina, ambapo licha ya kucheza vyema na kuwala chenga nyingi, Nigeria waliruhusu bao la Marcos Rojo dakika ya 85 na kutolewa.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo