Burudani

Khadija Kopa ampigia debe Diamond

0
Khadija Kopa ampigia debe Diamond
Khadija Kopa

Mkongwe wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Khadija Kopa amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumkabidhi ukumbi wa DDC Chang’ombe, mwanamuziki Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ ili aurekebishe na kuongeza kumbi za muziki.

Khadija Kopa alisema viwanja vya burudani vilivyokuwepo kwa sasa ni vichache, harafu bendi za upigaji muziki ni nyingi, hivyo ni bora kuwapa baadhi ya watu au wasanii wenye uwezo ili kuvikarabati viwanja vya zamani ili vitumike.

Alisema kama vikikamilika itasaidia sana wasanii kujipatia vipato, kwakuwa viwanja vitakuwa vingi, tena vikiwa katika sehemu tofauti tofauti.

“Mheshimiwa kuna kumbi ambazo hazitumiki, zinachakaa unaweza kumpa mtu kama Diamond akazikarabati na watu kufanya matamasha,” alisema.

Kopa kwa sasa anatamba na bendi yake mwenyewe ya Ogopa Kopa, ambayo inafanya vizuri katika muziki wa taarabu hapa nchini.

Soma pia:  Diamond aweka wazi hisia zake baada ya Kuachwa na Zari

Comments

Comments are closed.

More in Burudani