Burudani

Lulu Diva Amwaga povu lake

0
Lulu Diva Amwaga povu lake
Shilole (kusoto), Lulu Diva (kulia)

Mwanamuziki lulu Abassi maarufu kama Lulu Diva amewataka mashabiki wa muziki nchini kutoufananisha muziki wake na ule wa msanii mwenzake Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole ama Shishi baby.

Lulu Diva alisema kufananishwa kwa muziki wake na ule wa Shilole kunaweza kusababisha ugomvi ambao utaharibu kazi zake.

lulu diva
Lulu diva

Msanii huyo alisema kuna wakati mashabiki wanaweza kutengeneza uhasama kati ya mwanamuziki na mwanamuziki kwa kufananisha kazi zao jambo ambalo hataki litokee.

“Muziki wangu una ladha tofauti na ule wa Shilole, namuheshimu sana Shilole kama dada yangu kwani ameanza kufanya muziki kabla yangu hivyo sitaki mashabiki watugombanishe kwa kufananisha kazi zetu.” alisema Lulu Diva.

Mrembo huyo alisema anayetamba na singo ya ‘Mazoea’ alisema anawaomba mashabiki wake kuendelea kusapoti kazi zakena kuzipigia kura nyimbo zake ili ziendelee kufanya vyema kwenye chati za Bongo.

Soma pia:  Pierre Liquid kula shavu Marekani

Comments

Comments are closed.

More in Burudani