Burudani

Kardashian kuingia Gym baada ya kujifungua

0
kuingia Gym baada ya kujifungua
khloe kardashian

Mtayarishaji nyota  wa vipindi vya televisheni, Khloe Kardashian, amesema kwamba anatarajia kuanza kuingia gym kufanya mazoezi ya viungo ili kupunguza mwili.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, alisema kwamba anatarajia kuingia gym kufanya mazoezi ya viungo hivi karibuni baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mpenzi wake Tristan Thompson.

Alisema kwamba tangu ajifungue mwili wake unaongezeka kila kukicha na kwamba anataka kuingia gym ili kujiweka fiti ikiwa ni pamoja na kupunguza uzito.

Nyota huyo wa kipindi cha ‘Keeping Up with the Kardashians’, alisema kwamba anataka kuanza kufanya mazoezi maalum ili kuhakikisha anapunguza mwili haraka.

Vilevile, nyota huyo wiki iliyopita aliweka baadhi ya picha zake za zamani katika ukurasa wa Instagram na kuandika ujumbe mfupi kwamba anapenda kuona mwili wake huo unarudi tena.

Soma pia:  Nicki Minaj na Young Money wajiondoa tuzo za BET

“Ninatarajia kurejea kwenye mazoezi mfululizo ili kuhakikisha ninarejesha mwili wangu wa awali kwani kwa sasa nimeongezeka uzito kitu ambacho sipendi,” alisema nyota huyo.

khloe kardashian
khloe kardashian

Comments

Comments are closed.

More in Burudani