Michezo

Karate ya shotokan kufundishwa Zanzibar

0
Karate ya shotokan kufundishwa Zanzibar
Shotokan Karate

Chama cha Karate Zanzibar kinatarajia kufanya mafunzo ya mchezo huo aina ya shotokan kwa siku tatu kuanzia Februari 8-10 mwaka huu.

Mafunzo hayo yatasomeshwa na wakufunzi wapatao 10 kutoka Asia na Ulaya, katika ukumbi wa Judo uliopo uwanja wa Amaan mjini hapa.

Mwenyekiti wa chama hicho Abdalla Hussein ‘Sensei Dula’ alimwambia mwandishi wa habari hizi jana kwamba mafunzo hayo yatawashirikisha wanamichezo wa mchezo huo kwa rika zote wa ndani na nje ya Zanzibar.

“Tuna mafunzo hayo ni ya siku tatu ambayo yatashirikisha rika zote na pia na jirani zetu kutoka Kenya pamoja na ndugu zetu Tanzania nao watashiriki,” alisema.

Alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kufanya mahusiano ya kitaifa na kimataifa ili waendane na harakati za kilimwengu zilivyo.

Soma pia:  Saudia Arabia yakabidhi tani 100 za tende

Alisema katika mafunzo hayo zaidi ya washiriki 50 wanatarajia kushiriki ambapo watapata fursa ya kusoma masomo ya karate pamoja na Aikido.

Aidha alisema kwa washiriki wa mafunzo hayo watapaswa kujihudumia kwa mpaka kufika katika ukumbi huku chama kitahudumia maji na chakula.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo