Bondia wa Nchini Marekani Floyd Mayweather amesema yeye macho yake yapo kwenye fedha.
Amesema hawezi kupambana kama pambano litakuwa na fedha kidogo kwani hiyo ni kazi yake. Mayweather amesema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari nchini Marekani.
“Unajua ngumi ni mchezo hatari, kama mtu anaweza kutoa dola Milioni 300 kudhamini pambano langu na Conor McGregor aje,” alisema.
Tayari kuna tarifa kuwa Mayweather anaweza kupambana ulingoni na Conor McGregor kwa dola Milioni 210.
Comments