Michezo

Emmanuel Okwi: Ninataka Ubingwa ligi kuu bara

0
Ubingwa ligi kuu bara
Emmanuel Okwi

Mshambuliaji wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi ametoboa siri na kusema akili yake ni kuina timu yake ikitwaa Ubingwa ligi kuu bara.

Okwi alisema hafikirii sana kuchukuwa tuzi ya Mfungaji bora wa ligi badala yake anataka kuina timu yake ikichukua Ubingwa.

Nyota huyo anayeongoza kwa kuzifumania nyavy mara 18 msimu huu alisema hakuna kitu chochote anachotamani  sasa zaidi ya Ubingwa.

Alisema kuna wakati mchezaji anatamani kuifungia timu yake mabao mengi lakini kuna wakati anaona ni bora timu yake ipate matokeo mazuri hata yeye asipofuga, matokeo amabyo yanaweza kuisaidia kupata Ubingwa.

“Nikifunga au nisipofunga kwangu sio kitu kikubwa ninachotaka kukiona ni Simba inatwaa taji la Ligi msimu huu.

“Kuwa mfungaji bora wa Ligi kwangu hilo ni jambo la ziada, kikubwa ni kushirikiana na wachezaji wenzangu na kuhakikisha Simba inatwaa Ubingwa msimu huu,” alisema Okwi.

Soma pia:  Kauli ya Okwi kwa Simba, Okwi Kujiunga na Fujairah FC

Mganda huyo ametengeneza uelewani mzui na nahodha John Bocco na kuunda safu imara ya Ushambuliaji ambayo imzalishia Simba mabao 31 hadi sasa.

Okwi Ninataka Ubingwa
Emmanuel Okwi

Comments

Comments are closed.

More in Michezo