Michezo

Azam FC hali tete Kimataifa

0
Azam FC hali tete Kimataifa
Azam FC

Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pekee ndio unaweza kuisaidia Azam FC kucheza michuano ya Kimataifa Afrika mwakani.

Azam FC imeanza kuondoa matumaini ya kucheza michuano ya Kimataifa mwakani baada ya juzi kutolewa na Mtibwa Sugar katika michuano ya Kombe la FA.

Timu hiyo ilitolewa katika michuano hiyo kwa mikwaju ya penalti 9-8 baada ya sare ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo huo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema kwa sasa wana wakati mgumu kuhakikisha wanapambania nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa.

Alisema njia pekee ya kucheza michuano hiyo ni kutwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu hii jambo ambalo linaonekana gumu.

Soma pia:  Emmanuel Okwi: Ninataka Ubingwa ligi kuu bara

Azam FC inashika nafasi ya tatu katika Ligi kuu ikiwa na point 44 huku ikizidi michezo miwili Simba ambayo ina point 46.

Cheche alisema watahakikisha wanapambana vya kutosha ili kutwaa ubingwa na kupata nafasi ya kucheza michuano ya Kimataifa.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo