Burudani

Dogo Janja atangaza rasmi kuachana na Uwoya

0
Dogo Janja atangaza rasmi kuachana na Uwoya
Dogo janja alivyokuwa na Irene Uwoya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’ juzi alivunja ukimya wa muda mrefu baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kitendo hicho cha Dogo Janja ni kama kutangaza kuachana rasmi na aliyekuwa mkewe msanii wa filamu Irene Uwoya kwani kwa muda mrefu walikuwa wakificha kuachana kwao.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na habari kwamba Dogo Janja na Uwoya ndoa yao imefunjika, lakini wawili hao hawakuwa tayari kulizungumzia hilo kiundani zaidi ya kila mmoja kuonekana akifanya mambo yake mwenyewe.

“Hakuna neno linaloweza kutosha katika kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku ya kuzaliwa mpenzi wangu…Nifuraha kwangu siku ya kuzaliwa mpenzi wangu..mengine nitakuelezea chumbani.. Kula ushibe, Kisha kaza chaga… nakupenda sana” aliandika.

Soma pia:  Gigy Money - Mimina (Official Music Video)

Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya ilikuwa ya ghafla mwanzoni mwa mwaka jana, jambo lililoshangaza wengi huku wengine wakidai ilikuwa filamu, lakini wawili hao waliishi pamoja na mara kadhaa Dogo Janja alifanya mahojiano kwenye vyombo vya habari na kumsifia mkewe.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani