Top Stories

Bunge Japan laidhinisha bilioni 28/- kukabili majanga

0
Bunge Japan laidhinisha bilioni 28/-
Bunge japan

Bunge la Japan limepitisha bajeti ya ziada ya yen trilioni 3.04 sawa na Dola za Marekani bilioni 28 kukabiliana na majanga ya asili.

Imeelezwa bajeti iliyopitishwa awali kwa ajili hiyo ilikuwa yen bilioni 935.6 sawa na dola bilioni 8.53.

Pamoja na mambo mengine, fedha hizo ni za kuimarisha miundombinu ya umma. Katika bajeti hiyo mpya, yen trilioni 1.07 sawa na dola bilioni 9.86 zitatumika katika miradi ya kuimarisha maeneo yanayokumbwa na majanga kila mara, kuimarisha miundombinu ya barabara na kingo za bahari zilizoathiriwa na tufani na tetemeko la ardhi yaliyotokea hapo nyuma.

Imeelezwa yen bilioni 325.6 sawa na dola bilioni 2.97 zimetengwa kuwasaidia wakulima wa Japan kuongeza ushindani wao kutokana na nchi hiyo kuingia mikataba ya biashara huria.

Soma pia:  Mkutano kutatua mgogoro Libya

Serikali ya Japan imekusudia kufanya matumizi yake kulingana na ongezeko la mapato ya kodi.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories