Michezo

Benzema Afunga bao la 400 LaLiga

0
Benzema afunga bao la 400
Karim Benzema

Mchezaji wa Real Madrid, Karim Benzema, juzi alifunga bao lake la 400 katika mchezo wa ligi Kuu ya Hispania baada ya timu yake kushinda 3-0 dhidi ya Las Palmas.

Katika mchezo huo, Benzema alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 32, wakati mabao mengine yaliwekwa na Gareth Bale.

Benzema alisema kwamba anashukuru kufunga bao hilo na kuingia kwenye rekodi ya kufikisha mabao 400 kwenye Ligi kuu ya Hispania.

Benzema afunga bao la 400
Karim Benzema

Alisema amekuwa akipewa ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake, hivyo ana imani ataendelea kuipatia timu mabao zaidi.

“Nimefikisha idadi ya mabao 400, ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa kuendelea kunipa ushirikiano kila siku na kuingia kwenye rekodi mpya, nina imani ya kuendelea kufunga kila ninapopata nafasi,” alisema Benzema.

Soma pia:  Real Madrid yaanza vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya

Comments

Comments are closed.

More in Michezo