Michezo

Barcelona yamuongezea mkataba Valverde

0
Barcelona yamuongezea mkataba Valverde
Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 55 pia alikuwa na uwezo wa kuongeza mwaka mmoja kwenye mkatba wake ambao sasa utamfanya kuendelea kukinoa kikosi hicho mpaka mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020-21.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona alimbadili Luis Enrique Mei 2017 na kushinda taji la LaLiga na lile la Copa del Rey katika msimu wake wa kwanza.

Barca kwa sasa inaongoz aligi ikiwa na pointi 51 mbele kwa pointi sita dhidi ya wapinzani wake Real Madrid.

Valverde, ambaye awali mkataba wake ilikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu, ameiongoza timu hiyo kushinda mechi 65 kati ya 96 alizoongoza, akitoka sare mara 22 na kupoteza mechi tisa.

Soma pia:  Antoine Griezmann anatakiwa Barcelona

Comments

Comments are closed.

More in Michezo