Klabu ya Manchester United, imesema kuwa timu zitakazowahitaji nyota wake wawili, Paul Pogba na Romelu Lukaku zitalazimika kutoa jumla ya pauni milioni 200.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, amesema kuwa wanahitaji kiasi cha pauni milioni 200, kwajili ya kuwaachia nyota hao kuondoka kikosini msimu ujao.
Hata hivyo, kocha huyo alisisitiza kwamba Pogba atauzwa kwa pauni milioni 120 kutokana na ubora wake na lukaku gharama yake ni pauni milioni 80.
Wakala wa Pogba, Mino Raiola ameshaanza kufanya mazungumzo na klabu ya Real Madrid kwajili ya mteja wake kutia saini mkataba mpya kama wakifikia mwafaka taarifa iliyoandikwa juzi na gazeti la The Mirror.
Hata hiyo Juventus na Inter Milan zilionyesha nia ya kutaka kumsajili lukaku na hivyo kama wakifikia makubaliano atatimkia nchini Italia.
United huenda ikamuuza Pogba kwenda Real Madrid kwani imekuwa ikimuwania nyota huyo kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
Solskjaer alisema kuwa wanaweza kumuuza nyota huyo kwenda Real Madrid msimu ujao lakini uhakika utapatikana Ijumaa ya wiki hii kama ataondoka au ataendelea kubaki Old Trafford, Uingereza.
“Huwezi kumuwekea pingamizi mchezaji kama akitaka kuondoka na hiyo haikubaliki kwenye mchezo wa soka. Pogba amefanya mambo makubwa ndani ya klabu na kama ataondoka itakuwa ni heshima nyingine kwake kwajili ya kwenda kutafuta changamoto kwenye klabu nyengine.”
“Yeye ni binaadamu na kwamba ana maamuzi yake hivyo kama anataka kuondoka hatuwezi kumzuia kwani ameshafanya mambo makubwa ndani ya klabu yetu,” alisema kocha huyo.
Comments