Michezo

Martial amkubali zaidi Solskjaer kuliko Mourinho

0
Martial amkubali zaidi Solskjaer
Martial akiwa na Kocha wake Solskajaer

Anthony Martial amesema ni rahisi kucheza chini ya Ole Gunnar Solskjaer kuliko Jose Mourinho.

Martial amekuwa tegemeo kwenye ushambuliaji chini ya kocha wa muda Solskjaer, aliyeanza maisha yake Old Trafford kwa ushindi wa mechi 10 kati ya 11.

“Tumepata kocha ambaye yuko tofauti na tunajaribu kufanya yale anayotuelekeza,” alisema Martial ambaye alifunga bao lake la 11 msimu huu kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham mwishoni mwa wiki iliyopita. “Labda ni rahisi kucheza aina hii ya soka na si ile aliyoitaka [Mourinho].”

“Kocha wetu mpya ( Solskjaer) anapokuja huwa mwenye kujiamini, muwazi na hilo lilisaidia sana, tunajaribu kumlipa kwa anayotufanyia na mambo yanakwenda.”

“Aliniambia nishambulie sana, hiyo ni kazi yangu, baada ya yote kuwa tofauti, mambo yanakwenda kwa washambuliaji wengine na ninaimani tunaweza kuendelea kuwa vizuri.”

Soma pia:  Manchester United yakaribia kumsajili Dybala

Comments

Comments are closed.

More in Michezo