Michezo

Pogba amesema hana tatizo na Mourinho

0
Pogba na Mourinho
Paul Pogba

Nyota wa Man United, Paul Pogba amesema kwamba hana tatizo na  Kocha wake Jose Mourinho kama mashabiki wa soka wanavyofikiria.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakifikiria Mourinho na nyota wake Pogba kwamba wana tatizo kitu ambacho amekipinga vikali.

Paul Pogba mwishoni mwa wiki iliyopita, alipopanwa kwenye kikosi cha kwanza cha United kilichoivaa Swansea na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Nyota huyo amekuwa akikosa baadhi ya mechi na kuwafanya mashabiki kuanza kutabiri kwamba huenda kuna tatizo kati yake na Kocha Mourinho.

Pogba alisema kwamba anafurahia maisha kuendelea kuichezea Manchester United na hana tatizo lolote na kocha wake. pia aliongezea kwa kusema kwamba yeye na Mourinho wanaelewana vizuri tofauti na mashabiki wa soka wanavyofikiria.

Paul Pogba
Paul Pogba

Nyota huyo alisema kuwa atapambana katika kila mechi atakayocheza ili kuhakikisha anaisaidia timu yake kupata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kumaliza nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Soma pia:  Paul Pogba atamani kukipiga na Neymar

“Sina tatizo na kocha wangu Mourinho kwani kila kitu kinaenda vizuri, najitahidi kujituma kila wakati ili kuhakikisha timu inapata ushindi muda wote ninaopata nafasi ya kucheza,” alisema Paul Pogba.

Katika msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza, Manchester United ipo nafasi ya pili kwa point 68 nyuma ya vinara Manchester City yenye pointi 84 wakati Liverpool ipo nafasi ya tatu kwa pint 66.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo