Michezo

Mohamed Salah huenda akauzwa kwa dau kubwa

0
Mohamed Salah huenda akauzwa
Mohamed Salah

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Kloop amekiri kwamba huenda Mohamed Salah akauzwa.

Kloop alisema hayo wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo. Kocha huyo aliendelea kwa kusema kuwa mchezaji huyo ataendelea kuwemo ndani ya kikosi chake kwa mda wote aliosaini mkataba.

“Mohamed Salah ni mali ya Liverpool, anaweza kuondoka kwa vile zipo timu zinamtaka kwa dau kubwa mno,” alisema Kloop.

Mohamed Salah Kuuzwa
Mohamed Salah

Kauli hiyo ya kuondoka Salah imekuja siku chache baada ya kuwepo tetesi kuwa mchezaji huyo anawindwa na baadhi ya timu za Hispania na Ufaransa.

Soma pia:  Arsenal, Everton kumgombania Andre Gomes

Comments

Comments are closed.

More in Michezo