Michezo

Ujerumani warudi nyumbani vichwa chini

0
Ujerumani warudi nyumbani vichwa chini
Timu ya Taifa Ujerumani

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ujerumani juzi walirejea nyumbani wakiwa vichwa chini baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo.

Ujerumani juzi ilivuliwa rasmi ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Korea Kusini Kusini kwenye mchezo wa hatua ya makundi uluofanyika Uwanja wa Kazan.

Ujerumani jana walianza safari wakitokea Uwanja wa Ndege wa Vnukovo kwajili ya kurejea nyumbani huku wachezaji wakiwa hawaamini kile kilichotokea.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Low, alisema wanaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kutokana na kutolewa mapema kwenye fainali za mwaka huu. Alisema wanatambua kuwa wamewaudhi mashabiki hivyo wanaomba radhi kwani na wao waliumia baada ya kutolewa katika michuano hiyo.

“Tunaomba radhi mashabiki wa soka wa timu ya Ujerumani kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye fainali za mwaka huu, wachezaji walicheza chini ya kiwango na kusababisha tukatolewa mapema,” alisema Joachim Low.

Ujerumani Kombe la Dunia mwaka 2014
Kombe la Dunia 2014
Soma pia:  Maradona amsaka aliyemzushia kifo

Comments

Comments are closed.

More in Michezo