Burudani

Ray C kuolewa na mzungu Uingereza

0
Ray C kuolewa na mzungu Uingereza
Ray C

Mkongwe wa Bongofleva Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na kuanzisha familia na mpenzi wake anayeishi naye Uingereza.

Ray C alithibitisha tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo kwa sasa ana maisha mazuri baada ya kuchumbiwa na mzungu mwenye watoto wawili.

“Ukiona nipo London, ujue nipo kwa mchumba ukweli ni kwamba sijaolewa, lakini nina mchumba ambaye tupo kwenye taratibu za kufunga ndoa,”alisema Ray C.

Alisema anatamani kuzaa na mchumba wake na kwamba yupo kwenye mchakato huo na kinachosuburiwa ni ndoa ili kuzaa mtoto aliyedai kuwa na baraka zaidi.

Alisema, kazi alizoziachia mwaka jana zimeendelea kufanya vizuri na kuwataka mashabiki wake wasubiri kazi mpya.

Soma pia:  Drake kutengeneza kava la simu milioni 920

Comments

Comments are closed.

More in Burudani