Burudani

Ommy Dimpoz amsamehe Steve Nyerere

0
Ommy Dimpoz amsamehe Steve Nyerere
Ommy Dimpoz

Baada ya mwigizaji Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere kumuomba radhi msanii Ommy Dimpoz hatimaye amemjibu kwa kumwambia hana kinyongo naye na amemsamehe kwa hali zote.

Miezi kadhaa iliyopita Steve Nyerere alifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari na alisema kuwa Ommy Dimpoz asingeweza kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake.

Ommy Dimpoz alisema kuwa alishangazwa na kauli ya Steve Nyerere lakini baada ya kutambua kuwa alikosea hana budi kumsamehe na kuongeza kuwa bado anamheshimu hivyo wataendelea kushirikiana.

“Mimi kama nilivyosema mwanzo sina kinyongo na wewe, najua kama binadamu uliteleza na kuna kitu umejifunza na ningependa utambue bado nakuheshimu sana si unajua wewe ndo kiongozi wetu,” alisema Ommy Dimpoz.

Soma pia:  Q Boy Msafi: Kolelate - (OFFICIAL VIDEO)

Alisema kuhusu video ya Steve ambayo alitamka kuwa msanii huyo asingeweza kupona ataendelea kuiposti kwani imekuwa ikimfurahisha kila anapoitizama kwenye mitandao mbalimbali.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani