Imeelezwa kuwepo kwa uhaba wa viwanja vya kuchezea mchezo wa Pete mkoani Njombe ndio chanzo cha mchezo huo kudorora.
Pamoja na kukosekana kwa Chama cha mchezo huo ili kuhamasisha kumekuwa kukikatisha tamaa wachezaji wenye vipaji.
Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa mpira wa Pete waliozungumza wakati walipokutwa wakisaka uwanja wa kufanyia mazoezi ya mchezo huo, Walisema wamekuwa wakipata changamoto kubwa ya kupaat viwanja vya kucheza mchezo huo kwa madai kuwa uwanja wao wa awali uliokuwa ndani ya uwanja wa Sabasaba ulimegwa na kuwekwa jukwa la Watazamaji.
“Kikubwa kabisa tunachokabiliwa kwa Njombe ni uhaba wa viwaja tunatangatanga”. Alisema Irene Mwanuke.
Kwa upande wake Nahonda wa Timu ya Green Stars, Maria Mwafute, ambaye alisema wapo kwenye mazoezi ya maandalizi ya michuano ya Polisi jamii inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Naye Anita Ngole mchezaji nafasi GW, aliwataka wanawake wenzake kujitokeza kucheza mchezo huo kwajili ya kusaidia kufanya mazoezi na kuondokana na magonjwa nyemelezi.
Comments