Mashidano ya Urembo ya Miss Tanzania 2018 chini ya uongozi mpya wa Kampuni ya The Look yanaanza rasmi katika ngazi ya mikoa leo hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look Company, Basila Mwanukuzi, alisema Miss Tanzania 2018 yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Aprili 7, mwaka huu katika Ukumbi wa Makumbusho, jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa waandaaji, waratibu na wasimamizi wa mashindano hayo mikoa ya kwanza kufanya wiki hii itakuwa ni Dodoma na Mbeya.
Mwanukuzi alisema mikoa mingine iliyobaki itafanya mashindano yake kuanzia juni 7, mwaka huu huku mkoa wa mwisho kufanya shindano lake utakuwa ni Kinondoni, ambao utafanya shindano lake Julai 20.
Alisema baada ya mashindano ya mikoa kumalizika utakuwa wasaa wa kuanza ya kanda na yataanzia Nyanda za Juu Kusini, ikihusisha mikoa ya Rukwa na Mbeya.
Mwanukuzi alisema kanda hiyo itafanya shindano lake Julai 13, mwaka huu na watu wa mwisho kufanya shindano lao itakuwa Kanda ya Mashariki, itakayojumuisha mikoa ya Pwani na Morogoro, litakalofanyika mkoani Morogoro Agosti 4.
Comments