Michezo

Mbio za Ubingwa Ligi Kuu England kwampagawisha Guardiola

0
Ubingwa Ligi Kuu England
PEP Guardiola

PEP Guardiola amesema kitendo cha Manchester City kuwemo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England ni mafanikio.

Manchester City inatazamia kufuata nyayo za Manchester United walioshinda taji la England mara mbili mfululizo walipofanya hivyo mwaka 2008 na 2009.

Guardiola anaamini uwezo wa timu yake kuwa kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa na Liverpool, ni uthibitisho wa ubora wa timu yake.

“Najua miaka mitano au sita iliyopita kwenye mbio za ubingwa nini kiliwatokea na nafasi gani walikuwa,” alisema Guardiola. “Wote walikuwa kwenye mbio za ubingwa.

Hawakuwa na nafasi katika kipindi hicho kushinda taji la Ligi Kuu. Sisi tuna nafasi. Hicho ndicho ninachofurahia zaidi msimu huu.

“Wakati watu waliposema tuliwadharau Newcastle, haumdharau yoyote wakati unapofika fainali ya kombe la Carabao kwa mara nyingine tena na pia ukiwa uko kwenye mashindano yote.

Soma pia:  Pep Guardiola amuomba radhi Riyad Mahrez

“Chelsea, misimu mitatu iliyopita Leicester na wengine katika wakati kama huu hawakuwa na nafasi. Sisi tuna nafasi”. Hicho ndicho kinachonifurahisha.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo