Mwanamuziki Mariah Carey amesema kuna wakati anapenda kwenda kulala hoteli ili kubadili mawazo.
Mrembo huyo amelieleza Jarida moja la Nchini Marekani kuwa amekuwa anafanya hivyo pale anapopata muda. Alisema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuona jinsi gani watu wengine wanavyoishi.
“Pale najaribu kufuta mawazo niliyo nayo, lakini najua natumia fedha nyini nikiwa na walinzi wangu, bado najifunza jambo,” alisema.
Hata hivyo, Mwanamuziki huyo amesema ameweza kujifunza vingi ikiwemo jinsi gani ya kuimarisha penzi.
Comments