Michezo

Lucas Moura apiga hat trick ya kwanza Uwanja wa Tottenham

0
Lucas Moura hat trick Tottenham
Lucas Moura

Winga Lucas Moura wa Tottenham, ameweka rekodi ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ ya kwanza kwenye dimba jipya la Tottenham Hotspur, katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya vibonde walioshuka daraja, Huddesfield, jana mchana katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Tottenham walikuwa hapo katika pambano la tatu ndani ya uwanja huo mpya uliopewa jina la timu yaani Uwanja wa Tottenham Hotspur, ambako hiyo ni mechi ya pili ya EPL, baada ya kufungua na ushindi dhidi ya Crystal Palace na kicha kuichapa Man City katika Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi.

Katika mechi ya juzi usiku, ikiwakosa nyota wake wawili, Delle Alli na Harry Kane, Tottenham ilishuka dimbani kuwaalika Huddersfield, katika mtifuano uliotazamwa kama unaoweza uwa mgumu kwa wenyeji, lakini Moura akaufanya rahisi akifunga mara tatu, mbele ya watazamaji 58,308.

Soma pia:  Arsenal, Everton kumgombania Andre Gomes

Mabao yote ya Moura yalikuja baada ya bao la uongozi la Mkenya, Victor Wanyama dakika ya 24. Moura alitikisa nyavu katika dakika za 27, 87 na 90+3, kuipa ushindi uliowasogeza juu kutoka nafasi ya tano waliyokuwepo, hadi ya tatu wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 33.

Kikosi cha Tottenham katika mfumo wa 3-4-1-2, kilipangwa hivi: Lloris; Foyth, Sanchez, Vertonghen/Rose; Walker-Peters, Wanyama, Sis-soko/Skipp, Davies; Eriksen; Moura, Llorente/Son 87.

Kikosi cha Huddersfield katika mfumo wa 5-4-1, kilipangwa hivi: Hamer; Hadergjonaj, Schindler, Stankovic/Mooy, Kongolo, Durm/Mounie; Kachunga, Bacuna, Hogg, Lowe; Grant.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo