Msanii wa muziki wa kizazi kipya Linex Sunday (pichani) amesema anajutia kutoonana na msanii Golden Jacob ‘Godzillah’ ambaye amefariki dunia Jumatano ya wiki hii.
Linex alisema kutokana na alivyoguswa na msiba wa msanii huyo alijutia uamuzi wake wa kutotaka kuonana naye kabla ya hajafikwa na umauti.
Alisema alitaka kuonana naye siku tatu kabla ya kifo chake lakini alimuomba wakutane siku nyingine kwa sababu alikuwa na kazi nyingine.
“Niliongea na Zillah wiki moja kabla na alinitaka tukutane, wiki iliyopita alinipigia tena akaniomba nionane nae alipo lakini kutokana na ratiba zangu nilishindwa kukutana nae, sijui alitaka kuniambia nini,”alisema Linex.
Godzillah aliyekuwa akifanya muziki wa hip hop, alitarajiwa kuzikwa jana.
Comments