Michezo

Arsenal waibuka na Ushindi, Chelsea kilio EPL

0
Arsenal waibuka na Ushindi
Arsenal vs Stoke City

Mabao mawili ya Pierre-Emerick Aubameyang na moja la Alexandre Lacazette yameisaidia Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke City.

Arsenal ambayo ilipata ushindi huo katika dakika za lala salama kutokana na kubanwa mbavu na vijana wa Stoke City, baada ya ushindi huo Klabu ya Arsenal imesogea hadi nafasi ya 6 wakiwa na point 51.

Katika dakika ya 23′ kiungo Aaron Ramsey alitaka kuiandikia Arsenal bao la kwanza baada ya kupiga shuti kali ambalo liligonga mwamba.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, hakuna iliyoona lango la mwenzake ambapo ilimfanya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuingia kipindi cha pili na mikakati ya kushambulia zaidi kuliko kulinda.

Dakika ya 75′, Aubameyang alifunga  bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti baada ya Mesut Ozil kuchezewa rafu.

Soma pia:  Manchester United yakaribia kumsajili Dybala

Aubameyang aliongeza bao la pili katika dakika ya 86, akiunganisha krosi ya kona iliyookolewa na beki wa Stoke.

Katika dakika ya 89′, Lacazette aliifungia bao la tatu timu yake kwa mkwaju wa penalti, akitokea benchi.

Wakati huo huo, Chelsea nayo ilikuwa ikicheza dhidi ya Tottenham Hotspur, licha ya Chelsea kuanza kufunga, lakini Spurs waliibuka na ushindi wa bao 3-1.

Chelsea vs tottenham
Spurs wakisherekea ushindi

Comments

Comments are closed.

More in Michezo