Burudani

Albam mpya ya Neyo iko njiani

0
Albam mpya ya Neyo
Albam mpya ya neyo

Msanii wa muziki kutoka Marekani, Neyo anatarajia kutoa albam yake mpya inatayoitwa ‘Good Man’. 

Albam mpya ya Neyo inatarajiwa kuingizwa sokoni kwa mara ya kwanza tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu, Msanii huyo mara yake ya mwisho kutoa ilikuwa ni mwaka 2015.

Nyota huyo ambaye anatamba na wimbo wake ‘So Sick’, amesema kuwa albam yake imesheheni nyimbo bora na kwamba amewashirikisha wasanii wanaotamba nchini Marekani.

Neyo mwenye umri wa miaka 38, alisema kwamba albamu yake hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na maandalizi aliyoyafanya.

Msanii huyo wa Marekani juzi alitoa taarifa ya ujio wa albam yake mpya katika ukurasa wake wa twitter na kuweka baadhi ya vipande vya nyimbo.

Alisema kwamba ameamua kuitanguliza nyimbo yake mpya  inayoitwa ‘Push Back’ sokoni ili kuwapa kionjo mashabiki wake kuhusu albam yake mpya.

Neyo Push Back
Neyo: ‘Push Back’

“Nimefanya nyimbo nyingi lakini kwa sasa nimeamua kutoa albam mpya ambayo itaingia sokoni Juni 8 mwaka huu na kwamba mashabiki wakae tayari kuipokea kwani imesheheni nyimbo zenye ujumbe kwa jamii,” Alisema Neyo.

Soma pia:  Ibrahimovic Aanza makeke Marekani

Comments

Comments are closed.

More in Burudani