Burudani

Abdu Kiba arudi rasmi katika Muziki

0
Abdu Kiba arudi rasmi katika Muziki
Abdu Kiba Mubashara

Baada ya kimya cha muda mrefu, mwanamuziki wa kizazi kipya Abdul Kiba amesema Februari 14 amerudi rasmi katika muziki wa kizazi kipya kupitia wimbo wake mpya wa Mubashara.

Abdul kwa mara ya mwisho akiwa kama mwanamuziki huru, alisikika katika wimbo wa Jeraha ambapo baadaye alijiunga na kundi la King Music na kutoa wimbo wa Toto ambao ulikuja kuwatambulisha wasanii wapya akiwemo K-2ga, Killy na Cheed.

Alisema kwa sasa amerudi rasmi katika muziki akiwa na wimbo huo maalum kwa ajili ya Siku ya Wapendanao, huku akijiandaa kufanya kazi nyingi zaidi.

“Nanaanza upya safari yangu ya kimuziki. Tukutane kwenye vyombo vya habari kwaajili ya kunisikiliza nini naleta kwenye muziki, baada ya Mubashara,” alisema

Soma pia:  Rihanna na Jay Z waibuka tena pamoja

Comments

Comments are closed.

More in Burudani