Michezo

Rio Ferdinand kurejea Manchester United

0
Rio Ferdinand kurejea Manchester
Rio Ferdinand

Naibu Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Manchester United, Ed Woodward aamefunguka kuwa anapenda kuona Rio Ferdinand anakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Woodward amesema hayo jana wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari nchini Uingereza kuwa anaona gwiji huyo wa zamani ana uwezo wa kushika nafasi hiyo vizuri.

“Naona huyu ana uwezo wa kushika Ukurugenzi wa ufundi ili timu yetu iweze kufanya vizuri na kazi hiyo inamfaa kwa vile anaijua vizuri timu hii,” alisema Naibu Mwenyekiti huyo.

Ferdinand ni beki wa zamani wa Manchester United ambaye amefanya makubwa enzi zake zamani akiichezea timu hiyo pamoja na timu ya Taifa ya Uingereza.

Wakati kigogo huyo anaweka wazi juu ya Ferdinand kurejea kwenye dimba la Old Trafford, Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kumteua Mike Phelan kuchukua nafasi hio ya kuwa Mkurugenzi wa kiufundi.

Soma pia:  Manchester United kutinga nne bora

Comments

Comments are closed.

More in Michezo