Michezo

Pep Guardiola amuomba radhi Riyad Mahrez

0
Guardiola amuomba radhi Mahrez
Pep Guardiola akiwa na Riyad Mahrez

Pep Guardiola ameomba radhi kwa Riyad Mahrez kwa kutomtumia kwenye kikosi chake cha Manchester City kwa siku za karibuni.

Winga huyo wa Algeria ameanza mechi moja tu kwenye Ligi Kuu miezi miwili iliyopita, licha ya kuonekana kama angetumika kwenye mechi ya kombe la FA iliyotarajiwa kuchezwa jana dhidi ya Newport County.

Guardiola alisisitiza mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa ada iliyovunja rekodi klabuni hapo hajafanya lolote baya lakini hakuwa tayari kuwaacha wachezaji waliokuwa kwenye kiwango cha juu kama Bernardo Silva na Raheem Sterling.

“Mimi ndio sababu yay eye kutocheza,” Guardiola alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari. “Si kwamba yeye ndio anahusika na si kwamba ahisi sababu maalum ya kufanya hivyo.”

“Najisikia vibaya kwa sababu anafanya vizuri kwenye mazoezi, ni mchezaji mwenye kipaji lakini kwa wakati huo tuna washambuliaji watano, kwa mfano katika mechi za mwisho Leroy [Sane] hakucheza. “Tuna wachezaji wengine wazuri, kama kwa mfano Bernardo na Raz wako kwenye kiwango cha juu na hiyo ndio sababu yenyewe, hakuna sababu nyingine.”

Soma pia:  Tetezi juu ya Uhamisho wa Riyad Mahrez

“Ni mtu mzuri, tunafuraha kuwa nae, lakini kwa bahati mbaya zikuwa mzuri kwake kutokana na ukweli kwamba sijampa dakika anazostahili kucheza, naomba radhi, hilo ndio ninaloweza kusema.”

Comments

Comments are closed.

More in Michezo