Michezo

Ushindi wa Spurs dhidi ya Dortmund Ligi ya Mabingwa Ulaya

0
Spurs Ligi ya Mabingwa Ulaya
Ushindi wa Spurs dhidi ya Dortmund jana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya

Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino amesema kuwa “watu wanatuchukulia poa” na sasa wanatuita “mashujaa” baada ya kuwafunga vinara wa Ligi Kuu ya Ujerumani ya Bundesliga Borussia Dortmund 3-0 katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya 16 bora.

Son Heung-min, Jan Vertonghen na Fernando Llorente kila mmoja alifunga bao wakati Spurs ikitawala kipindi cha pili cha mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Wembley.

“Timu inapambana. Majivunia sana hilo, “alisema Pochettino. “Wanastahili sifa zote. Walichofanya ni kitu cha aina yake.”

Spurs imefanya kile ambacho hakikutarajiwa cha kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya mtoano ya mashindano hayo baada ya kujipatia pointi moja kutoka katika mechi zake tatu za makundi.

Walicheza mchezo huo bila ya kuwa na mfungaji wao mahiri Harry Kane na kiungo Dele Alli kwenye uwanja wa Wembley Jumatano lakini bado wameweza kuifunga Dortmund ambayo kikosi chao kimeweza kucheza mara tano katika misimu sita iliyopita hatua hii ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Soma pia:  Mbio za Ubingwa Ligi Kuu England kwampagawisha Guardiola

Son ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Korea Kusini, ambaye amefunga mabao manne katika mechi kibao tangu aliporejea kutoka katika mashindano ya Kombe la Asia, ameisaidia sana Tottenham baada ya kufunga bao la kwanza,” alisema Pochettino.

“Son amekuwa mtamu tena. Nafikiri ni mchezaji ambaye anaipatia mambo kibao,” alisema Pochettino. “hutabasamu na ni mchezaji mwenye nguvu. Kiwango chake kimekuwa kikiongezeka kila mchezo.”

Licha ya ushindi mnono katika mchezo wa kwanza, Pochettino bado anaamini kuwa kuna kazi ya kufanya ili kusonga mbele na kucheza robo fainali.

Mchezo wa marudiano umepangwa kuchezwa Machi 5 huko katika mji wa Dortmund wa Westfalenstadion nchini Ujerumani.

“Ushindi wa mabao 3-0 ni matokeo mazuri lakini wakati huohuo nafikiri tunahitaji kumalizia kazi tuliyoianza, “aliongeza Pochettino

Comments

Comments are closed.

More in Michezo