Burudani

Drake amaliza bifu kiaina na Kanye West

0
Drake bifu na Kanye west
Drake na Kanye west

Kila mmoja anafahamu Drake yupo kwenye bifu kali na Kanye West kwa muda mrefu lakini alichokifanya Drake juzi kimewafanya watu kuwa na sitofahamu kwamba chuki baina yao imekwisha au nini kimetokea.

Drake ameamua kukumbuka alipotoka kwa kutoa shukrani kwa kila mmoja aliyechangia yeye kufika hapo kipindi ambacho hakuna aliyekuwa akimfahamu.

Kati ya aliowashukuru, Kanye naye yupo akimshukuru kwa dhati kwa kutengeneza mixtape yake ya So Far Gone ambayo sasa imefikisha miaka 10.

Wengine aliowashukuru ni Trey Songz, Omarion aliyekubali kuimba katika wimbo wa Drake aliyekuwa hafahamiki na mtu yeyote wakati huo.

LeBron James, Bun B, Boi-1da na wengine wametajwa katika shukrani hizo alizoziandika wazi mwanamuziki huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram

Soma pia:  Tuzo za Grammy 2019 zapata pigo

Comments

Comments are closed.

More in Burudani