Burudani

Rayvanny aweka rekodi wimbo wa Tetema

0
Rayvanny aweka rekodi wimbo wa Tetema
Rayvanny wimbo wa Tetema

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Raymond Shaban maarufu Ray Vanny ameingia katika rekodi za wasanii wachache baada ya wimbo wake wa tetema kutizamwa na watu milioni moja ndani ya masaa 17.

Ray Vanny aliweka rekodi hiyo juzi na kushindwa kuvunja rekodi iliyowekwa na msanii Diamond baada ya wimbo wake wa Hallelujah kutizamwa na watu milioni moja ndani ya msaaa 15 pekee.

Baada ya kuweka rekodi hiyo msanii huyo aliwataka mashabiki wake kuendelea kuutizama wimbo huo ambao pia ulisifiwa na Naibu Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza.

Msanii huyo sasa anakuwa wa pili nchini baada ya Diamond ambaye wimbo wake umetizamwa mara nyingi ndani ya muda mchache huku bado ukiendelea kufanya vizuri na hadi sasa umetizamwa mara milioni mbili.

Soma pia:  Drake kutengeneza kava la simu milioni 920

Msanii wa tatu ni Ali Kiba ambaye aliweka rekodi hiyo baada ya wimbo wake wa Seduce me kutizamwa kwa idadi hiyo ndani ya masaa 37 katika mtandao wa Youtube

Comments

Comments are closed.

More in Burudani