Burudani

Shoo ya Ali Kiba yafunika Muscat Oman

0
Shoo ya Ali Kiba yafunika Muscat
Shoo ya Ali Kiba Muscat, Oman

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba juzi alifunika katika shoo aliyoifanya Muscat Oman.

Hiyo ilikuwa shoo ya kwanza kubwa kwa msanii huyo tangu kuanza kwa mwaka huu baada ya kufanya vizuri mwishoni mwa mwaka jana ambapo alifanya shoo katika mikoa kadhaa na nje ya nchi.

Vipande vya video vilivyokuwa vikizunguka jana kwenye mitandao ya kijamii vilimuonyesha Kiba akiwa kapagawa na umati wa mashabiki wake waliofurahia muziki wake uliokuwa ukiimbwa ‘live’ jukwaani.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake wa kadogo alioutoa mwanzoni mwa mwaka huu na ambao unafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya runinga, redio na mitandao ya kijamii.

Kiba ni miongoni mwa wasanii nyota nchini wanaofanya vizuri kwa muda mrefu na sasa ameajiri wasanii katika lebo yake ambao wanatamba na wimbo wa Mwambie Sina.

Soma pia:  Ray C kuolewa na mzungu Uingereza
Shoo ya Alikiba Muscat

Comments

Comments are closed.

More in Burudani