Michezo

Serengeti Boys dimbani Kesho dhidi ya Uganda

0
Serengeti Boys dhidi ya Uganda
Serengeti Boys

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 kesho itashuka dimbani katika mchezo wake wa kwanza na mashindano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati.

Kikosi hicho kitashuka dimbani kupambana na timu ya Uganda, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Muyinga mjini Bunjumbura, Burundi.

Michuano hiyo, imeandaliwa na Baraza la vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Kikosi hicho kiliondoka Dar es salaam juzi kwenda Burundi tayari kwa mashindano hayo kikiwa na Wachezaji 20 chini ya kocha Mkuu Kim Poulsen.

Soma pia:  Simba, Azam macho yote CECAFA Kagame

Comments

Comments are closed.

More in Michezo