Makala

Ni Unyama mwanzo mwisho Liberia – Johnny Mad Dog

0
Jonny Mad Dog
Filamu ya Jonny Mad Dog

Kikundi cha askari-jeshi watoto waliojiunga na kundi la waasi nchini Liberia la Liberians United for Reconciliation and Democracy (LURD) linafanya unyama mwaka 2003, mwishoni mwa Vita ya Pili ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Askari watoto – kama walivyo askari watu wazima, wako makini, wana nguvu, wana utii na wako tayari kupokea amri, wanaweza kutumia silaha, na wanajitoa mhanga tofauti na watu wazima.

Kijana mmoja wa Liberia aliyepewa jina ‘Kapteni Muuaji’ aliwahi kujigamba kuwa: “Watu wazima walipoogopa na kukimbia, sisi watoto tulibaki na kuendeleza vita.” Katika filamu hii kiongozi wa muasi, Johnny Mad Dog mwenye umri wa miaka 14 anaongoza kikundi kidogo cha wavulana wadogo wakiwa chini ya Jenerali mkongwe, Never Die, anayewapa cocaine kama kiburudisho.

Filamu inafuatilia maandamano ya kikundi hiki kuelekea mji mkuu wa Monrovia, inaonesha jinsi wanavyopita miji na vijiji kadhaa, wanavyosababisha taharuki na vitisho kwa jamii na mara kwa mara kuua watu.

Soma pia:  Eden Hazard ni Mlevi wa Filamu

Wanajeshi hawa watoto wanafanya unyama, vitendo vya uharibifu na ubakaji, na wakati mwingine bila hata kujali sana maisha yao wenyewe.

Ni kikundi cha vijana wenye umri wa miaka kati ya 10 na 15, kila mmoja amebeba bunduki, wakiwa wana mzuka wa kushambulia mji mkuu. Huu ni ulimwengu wa wapiganaji watoto barani Afrika unaooneshwa katika filamu ya kivita yenye ukatili na inayosisimua ya Johnny Mad Dog, iliyotengenezwa mwaka 2008, na kuongozwa na Jean-Stéphane Sauvaire.

Filamu imetokana na riwaya ya mwaka 2002 inayoitwa Johnny Chien Méchant, iliyoandikwa na mwandishi wa vitabu wa Congo, Emmanuel Dongala anayeishi nchini Marekani.

Nguvu ya filamu hii ipo katika ushawishi wake kuwa watoto wanaweza kufanya kazi ya watu wazima, ikiwa ni pamoja na uharibifu na ubakaji. Baadhi yao wana mambo ya ajabu ya kitoto: mmoja ana mabawa kama malaika, mwingine anavaa shela la harusi ya mwanamke ambaye mume wake ameuawa.

Soma pia:  Ifahamu filamu ya Armageddon (1998)

Wanatumia majina ya utani kama vile Captain Dust to Dust, Chicken Hair, Small Devil na Jungle Rocket. Anayeinogesha zaidi filamu hii ni Johnny Mad Dog, nafasi iliyochezwa na Christopher Minie, mwenye umri wa miaka 14 ambaye ndiye kiongozi wa kundi.

Wa pili kwa ukuu ni mvulana mdogo mwenye kiu ya kumwaga damu anayeitwa No Good Advice. Misheni yao kubwa ni kuendeleza vita vijijini na mijini, “kushikilia nafasi” na kuwatisha watu, kulazimisha watoto wote kujiunga nao na kuiba chakula na fedha.

Wameruhusiwa kuua raia kwa silaha na kazi yao nyingine ni kuvutia wadunguaji waliowekwa na jeshi la serikali. Mzuka unawapanda, wanaendelea kupigana, ukiwaona utadhani ni uwanja wa michezo ya kuzimu.

Hata hivyo wana umoja na mkakati. Hadithi ya Johnny inafunguka sambamba na ile ya msichana mdogo aitwaye Laokole, nafasi iliyochezwa na Daisy Victoria Vandy, akiwa sehemu ya raia wanaokimbia mapigano, lakini yupo tayari kukabiliana na Johnny.

Soma pia:  Eden Hazard ni Mlevi wa Filamu

Laokole anamsafirisha baba yake mgonjwa katika toroli na wakaati huo huo lazima amlinde mdogo wake. Anashuhudia kundi la Johnny likimuua kwa risasi kijana mdogo. Mara, Johnny na Laokole wanakutana kwenye ngazi iliyopasuka katika jengo lililotelekezwa.

Wanatazama machoni. Na kuanzia wakati huo, kuna kitu kinaonekana kuanza kujengeka ndani ya Johnny. Je, Laokole anaweza kumbadilisha Johnny? Hilo litakuwa rahisi sana.

Hata hivyo, kuna kitu kinatokea, ambacho kinamchukua Johnny na kumtupa nje ya dunia iliyofungamana na mauaji.

Comments

Comments are closed.

More in Makala