Makala

Baking soda tiba ya Kusafishia sehemu chafu bafuni

0
Kusafishia sehemu chafu bafuni
Usafi Bafuni

Kusafisha bafuni ni moja ya kazi isiyofurahiwa sana, lakini lazima kusafishwe. Kibaya zaidi unajikuta ukiishia kufanya usafi kwa bidhaa mbalimbali za kusafishia kila eneo katika bafu lako kuanzia bakuli la choo, hadi sinki, mkaragazo (shower) hadi sakafu.

Bahati kuna njia rahisi ya kukabiliana na usafi wa bafu nayo ni: baking soda! Katika dondoo zifuatazo utapata muongozo wa namna ya kutumia kusafisha sehemu korofi za uchafu bafuni kwako.

Mifereji ya maji (drains):

Mifereji ya maji ni moja ya sehemu janja (na mara nyingi inatia kinyaa) unayobidi kusafisha. Hata hivyo ukitumia baking soda ni njia salama na bora zaidi kusafishia mifereji yako na kuiacha ikinukia vizuri.

Mimina nusu kikombe cha baking soda kwenye mfereji wa maji na acha itengeneze mapovu. Acha kwa dakika 10 kabla ya kumimina maji moto kwenye mfereji.

Soma pia:  Mradi wa Pasipoti ya Kielektroniki pamoja Faida zake

Mazulia ya bafuni:

Kwa kuwa hurowa maji na hayapati muda wa kukauka vizuri, ni rahisi kutengeneza madoa na harufu. Yasafishe kwa kwa kutumia nusu kikombe cha baking soda.

Mapazia yanayofunika bomba la mvua (shower curtains):

Kama una mapazia yanayoosheka basi yafue pamoja na mazulia ya bafuni na changanya na baking soda kung’arisha zaidi.

Kama una mapazia ya plastiki nyunyizia baking soda kwenye sponji lenye unyevuunyevu na kisha sugua mapazia yako. Kisha yazuuze na kazi yako imekamilika.

Sakafu na niru:

Sakafu ni moja ya sehemu zinazohitaji usafi mno bafuni kwako. Lakini bila kutumia nguvu kusugua na kutumia kemikali kali unaweza kuwa na mistari ya niru misafi.

Changanya nusu kikombe katika maji ya uvuguvugu, kisha piga deki sakafu na usafishe vizuri. Kusafisha mistari ya niru, tumia brashi dogo au mswaki kupaka mchanganyiko huo kwenye mistari ya niru na sugua kuiweka safi.

Soma pia:  Historia ya Intaneti, Mambo 16 huenda ulikuwa huyajui kuhusu Intaneti

Vikapu vya uchafu:

Vifanye vikapu vyako vya bafuni kuwa freshi kwa kunyunyiza baking soda. Lakini pia kila unapotoa uchafu kwenye kontena la taka, lisafishe kwa kutumia mchanganyiko wa galoni moja la maji na kikombe kimoja cha baking soda.

Kusafishia sehemu chafu bafuni Baking Soda
Usafi Bafuni

Comments

Comments are closed.

More in Makala