Makala

Historia ya Hayati Abeid Amani Karume

0

Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, jana alitimiza miaka 46, tangu alipopatwa na umauti baada ya kupigwa risasi. Sheikh Karume alipigwa risasi April 7, mwaka 1972 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM eneo la Kisiwandui visiwani Zanzibar.

Alipigwa risasi wakati akicheza mchezo wa bao na wenzake, ambapo aliyemuua naye aliuawa papo hapo na walinzi wa Karume, baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Karume day

Hayati Karume

Historia ya Hayati Abeid Amani Karume;

Alizaliwa mwaka 1905, hivyo hadi umauti unamfika alikuwa na umri wa miaka takriban 67, huku umauti huo ukimfika akiwa katika eneo la michezo ambalo ni sehemu ya kucheza bao.

Wataalamu wa michezo wanaeleza mchezo wa bao ni miongoni mwa michezo inayotumia akili nyingi, katika kupata ushindi dhidi ya mpinzani wako, ikilinganishwa na michezo mingine

Tunaweza kusema moja kwa moja ni mwanamichezo aliyepoteza maisha wakati wa michezo kitu ambacho ndicho kilikuwa kipenzi chake katika kupumzisha akili yake baada ya majukumu yake ya kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Mbali na siasa ambayo watu wengi ndiyo wanamfahamu, lakini alikuwa ni mwanamichezo mahiri akishiriki katika kucheza na kuchangia katika shunguli za michezo ambazo zimekuwa zikichangia kuwapa ajira vijana.

Historia zinamtaja Karumekuwa, kabla ya kujikita katika harakati za siasa alifanya kazi ya Ubahari iliyomwezesha kuzunguka nchi nyingi duniani.

Inaelezwa katika kipindi hicho cha ujana wake, alianzisha timu ya mpira wa miguu iliyofahamika African Sport ya visiwani Zanzibar, huku mwenyewe alikuwa Mchezaji wa timu hiyo.

Serikali za kikoloni zilikuwa zinaruhusu vyama vya kijamii na michezo na kupinga uanzishwaji wa vyama vya siasa.

Inaelezwa katika mikusanyiko ya kimichezo walitumia mwanya huo katika kujadili jinsi ya kujikomboa kutoka katika makucha ya wakoloni.

Anakumbukwa ‘kuzipiga Jeki’ yanga na simba;
Karume Yanga na Simba

Yanga S.C na Simba S.C

Mwaka 1970 Rais Karume aliialika timu ya Yanga, katika Ikulu ya Zanzibar kufanya nayo mazungumzo.

Inaelezwa wakati huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa timu hiyo ni Hayati Tabu MAngara, alimueleza juu ya matatizo ya timu hiyo ikiwemo ya timu hiyo kutokuwa na uwanja wa mazoezi pamoja na jengo lake.

Mwaka 1971, Karume baada ya kusikia kilio hicho, anadaiwa aliwapatia kiasi cha fedha za ujenzi wa jengo la timu na uwanja wa Kaunda uliokadiriwa kuingiza watazamaji 14,000.

Katika Klabu ya Simba, alishiriki katika kupatikana kwa eneo la kujenga ujenzi wa jengo la timu hiyo hadi kufanikiwa kukamilika kwa kutoa fedha pia.

Vivyohivyo, anatajwa kuwa ndiye chachu ya timu hiyo kuitwa jina la Simba, baada ya awali timu hiyo kuitwa Sunderland Sports Club.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali alisema jana kuwa Karume alikuwa shupavu wa Klabu hiyo, wakati huo kubadilisha jina, kwani jinahilo lilikuwa likitukuza ukoloni badala ya utamaduni wa Kiafrika.

Ikumbukwe kipindi hicho, vuguvugu la Ukombozi wa Bara la Afrika na Uzalendo vilikuwa vimepamba moto nchini na nchi za Afrika kwa ujumla.

Hata hivyo, alipendekeza timu hiyo iitwe Simba Mwekundu Sports Club, jina ambalo alisema linaendana na utamaduni wa nchi yetu.

Viongozi wa Simba, kwa wakati huo walikubaliana na ushauri huo na Klabu hiyo ikaanza kuitwa jina hilo jipya hadi leo ikifahamika kwa jina la Simba,

Kimsingi, Hayati Karumeana historia iliyotukuka katika michezo, kiasi cha Uwanja zilipo ofifi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuitwa uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Basi kutokana na mchango wake katika medani ya michezo wanamichezo tunapswa kumkumbuka Hayati Karume, kwa mchango wake alioutoa katika medani ya mchezo.

Kiongozi huyo, hakuishia hapo, alifanikisha ujenzi wa Uwanja wa Amani kule visiwani Zanzibar.

Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina alisema jana kwamba wanamkumbuka Mzee Karume kwa mengi katika soka.

“Ukweli moja ni kutoa mchango wake mkubwa wa Ujenzi wa Uwanja wa Amani, huyu alikuwa kiongozi mahiri, tutaendelea kumuenzi daima,” alisema kiongozi huyo.

Lakini kwa ujumla, mafanikio hayo, yamechangia kuazishwa kwa timu nyingi visiwani humo na vijana wengi sasa hivi wanapata ajira kupitia michezo.

Tunamuomba Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Ameen.

Mwalimu Nyerere na Hayati Karume

Picha: Mwalimu Nyerere (Kushoto) na Hayati Karume (kulia)

Hayati Abeid Amani Karume

Hayati Karume

Comments

Comments are closed.

More in Makala