Makala

Fahamu namna ya kukabili moto wa jikoni

0
Namna ya kukabili moto wa jikoni
Moto wa jikoni

Moto unaoanzia majikoni mara kadhaa umekuwa sababu ya nyumba mbalimbali kuungua.

Kuna sababu mbalimbali zinazosababishwa na moto huu kuungu za majumba ikiwa ni pamoja na wahusika kukosa elimu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto lakini kubwa ni uzembe.

Uzembe mara nyingi hutokea pale mtu anapoacha shughuli za mapishi zikiendelea na kwenda kujishughuli na mambo mengine kama vile kwenda sebuleni kuangalia runinga ama kuchezea simu na mengine kama hayo. Kimsingi upishi unapaswa kusimamiwa kwa umakini muda wote.

Kwa kuacha ‘jiko likijipika’ bila usimamizi, inaweza kusababisha kile kinachopikwa kuungua kwa kukaa muda mrefu jikoni na kusababisha moto kuanza kutokea.

Je, moto ukitokea unatakiwa kufanya nini? Kwanza kabisa unachotakiwa kufanya ni kutoa taarifa haraka kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kupiga simu ya dharura namba 114 na kutoa maelezo sahihi ya mahali tukio la moto lilipo. Ni vyema pia watu kujenga tabia ya kuorodhesha namba muhimu kama hiyo kwenye simu zao kama hawawezi kuzikariri vichwani.

Ukishapiga namba hiyo, eleza ni kitu gani kinaungua na ni vvema ukatoa namba ya mawasiliano ili kulirahisishia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufika eneo la tukio kwa urahisi kutokana na hali halisi ya miundombinu ya miji ilivyo hapa nchini.

Baada ya kuwasiliana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unatakiwa kuchukua kizimia moto ambacho kinafaa kwa kuzimia moto kwenye jiko ili uweze kuudhibiti kwa haraka kabla haujawa mkubwa na kuleta madhara makubwa kwenye nyumba.

Moja ya njia bora na salama ya kuzima moto wa jiko unaweza kutumia nguo nzito kama vile taulo kubwa lenye asilimia 100 ya pamba, hakikisha taulo hilo lisiwe jembamba na liwe na unene wa kutosha au unaweza kutumia shuka lakini kumbuka kuiloweka katika maji kisha uikamue halafu uikunje zaidi ya mara moja ili kuiimarisha kwa kuiongezea unene na hivyo kuifanya kuwa madhubuti zaidi, kisha funika sehemu inayowaka moto jikoni.

Soma pia:  Mradi wa Pasipoti ya Kielektroniki pamoja Faida zake

Lengo la hatua hii ni kuzuia hewa ya Oksijeni kwenye sehemu inayowaka moto ili hewa hiyo isiendelee kuchochea kuwaka kwa moto na hapo utakuwa umeweza kuudhibiti moto kirahisi kama utakuwa hauna vizimia moto maalumu vinavyotakiwa kuwekwa eneo la jikoni.

Vilevile unaweza kutumia chumvi kama moto unawake ndani ya sufuria au kikaangio ili kuupunguza kasi na kuudhibiti kabisa au unaweza kutumia mfuniko au sinia kwa kufunika juu ya sufuria au kikaangio kwa lengo la kuzuia hewa ya oksijeni isiweze kuchochea moto kuzidi kukua na kuleta athari kubwa kwenye nyumba.

Mara kwa mara pendelea kuweka taulo au nguo nzito eneo la jikoni. Ni vyema iwe sehemu ambayo utaifikia kwa urahisi pale ajali ya moto inapotokea na kuweza kuitumia. Hii itasaidia kama hauna blanketi maalumu la kuzimia moto (fire blanket) katika eneo la jiko lako kwa tahadhari ya ajali ya moto.

Mbali na tahadhari hiyo, jambo lingine ni kufanya usafi wa kutosha jikoni kwako kwa kuhakikisha hakuna matone ama michirizi ya mafuta ya taa au mafuta ya kupikia ili kuzuia yasiwe sababu ya kulipusha na kusam-baza moto zaidi endapo utatokea.

Hili pia linaepusha ajali nyingine ya kusababisha mtumiaji wa jiko kuteleza na kuanguka sakafuni. Mara nyingi moto unapotokea jikoni usipende kuukadiria kuwa unaweza kukua na kusambaa kwa kiwango gani, bali kumbuka kutumia taulo, nguo nzito ama blanketi maalumu haraka kuuzima.

Soma pia:  Top 5 ya Wachezaji ghali zaidi duniani 2017/2018

Hakikisha kufunika sehemu inayoungua moto pasipo kutaharuki ili hewa ya oksijeni isiweze kuingia na kusababisha moto kuendelea kuwaka.

Baada ya kufunika vizuri sehemu iliyokuwa inaungua moto unatakiwa kuzima jiko husika mara moja. Kama ni jiko la mafuta ya taa unatakiwa ushushe tambi za jiko, kama ni jiko la umeme unatakiwa uzime swichi ya umeme (switch socket) na kama ni jiko la gesi hakikisha unafunga valvu ya mtungi wa gesi, na kuendelea kufanya mawasiliano na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kama bado una mashaka na tukio hilo.

Vilevile unaweza kutumia taulo zaidi ya moja ili mradi uweze kuudhibiti moto kiurahisi, lakini kumbuka usitumie taulo lenye maji maji kwenye jiko la umeme kwa sababu maji ni kipitisha umeme rahisi na hivyo linaweza kumuathiri mtumiaji kwa kupigwa na shoti ya umeme.

Kama taulo au nguo imelowa maji kwenye jiko la umeme hakikisha umezima umeme kwanza ndipo utumie taulo au nguo yenye umajimaji kama hutokuwa na blaketi maalumu la kuzimia moto.

Ni muhimu kuweka jikoni kizimia moto aina ya hewa ya ukaa (CO2 Portable fire extin-guisher). Kizimia moto hiki ndio bora zaidi kwa kuwekwa jikoni kwa kuwa kina zima moto kwa urahisi na hakina madhara yeyote kwenye chakula eneo la jikoni na pia hakichafui mazingira. Halikadhlika ni kizimia moto ambacho hakipitishi uememe kirahisi na kumwathiri mtumiaji.

Pamoja na umuhimu wa kuweka kizimia moto cha hewa ya ukaa kwa eneo la jikoni pia muhimu kufunge kifaa cha kung’amua moto au king’amuzi joto (heat detector) na blanketi maalumu la kuzimia moto (Fire Blanket).

Soma pia:  Jinsi ya kupata Passport mpya ya Kielektroniki

Vifaa hivi vyote vinapaswa kuwekwa eneo la jikoni ili kugundua moto mapema na kukuwezesha kuudhibiti haraka pindi kabla haujaleta madhara makubwa.

Kamwe usitumie vitu kama sponji, mito au dawa za kuulia mbu kwa lengo la kuzima moto kwani vitu hivyo ni rahisi kushika moto na kuusambaza na kuleta matokeo ya moshi mzito ulioambatana na sumu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha madhara kwako ukizivuta.

Zingatia kupata ushauri kwanza kabla ya kuweka vizimia moto au ving’amuzi vya moto katika eneo lako la jikoni ku-toka kwa wataalamu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ili upate muongozo stahiki.

Kutegemea na jiko lake utashauriwa kuweka ving’amuzi vya moto vya aina gani na ukubwagani.

Vile vile zingatia kabla ya kujenga nyumba ipeleke ramani yako ya nyumba unayotarajia kuijenga karibu na kituo cha zimamoto kwa lengo la kupewa ushauri wa kinga na tahadhari za majanga ya moto kwa kushauriwa kuhusu moshi, ving’amuzi vya moto na vizimia moto.

Hatua hii ni muhimu kujiandaa kabla ya janga la moto kutokea na nini cha kufanya pindi ajali ya moto itakapotokea ili kuokoa maisha na mali.

Kumbuka: “Iwapo umez-ingirwa na moshi, tambaa kwa kutumia magoti na mikono. Kumbuka pia hairuhusiwi kurudi ndani ya jengo linalowaka moto hadi hali itakapokuwa salama ku-fanya hivyo au utakaporuhusiwa na ofisa wa Jeshi la Zimamoto.

Comments

Comments are closed.

More in Makala