Michezo

Guardiola amtetea Sarri na kipigo

0
Guardiola amtetea Sarri na kipigo
Pep Guardiola

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemhurumia mwenzake wa Chelsea, Maurizio Sarri na kusema kuwa anatakiwa apewe muda zaidi ili aweze kuinoa vizuri timu hiyo.

Man City iliisambaratisha Chelsea kwa mabao 6-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad juzi, kikiwa ni kipigo kikubwa zaidi kuwahi kufungwa Chelsea katika mashindano yoyote tangu mwaka 1991 na kikiwa ni kipigo kibaya zaidi kuwahi kukipata kocha huyo Mtaliano akiwa kama kocha wa kulipwa.

Hata hivyo, Guardiola alimtetea Sarri – ambaye alichukua nafasi ya Antonio Conte kama kocha katika klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge katika kipindi cha majira ya joto, akielezea kuhusu yeye alipokuwa akipambana katika msimu wake wa kufundisha timu ya Ligi Kuu na kufungwa na Chelsea 2-0 Desemba.

Soma pia:  Liverpool yamtaka kumsajili lorenzo wa Napoli

Kocha huyo wa City pia alidokeza mazuri aliyofanya Sarri wakati akiifundisha Napoli, ambayo City ilicheza nayo msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, na kushauri kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 anahitaji huruma kutoka kwa wamiliki ili kuipeleka mbele Chelsea.

Alipoulizwa kama ana huruma na Sarri, Guardiola alisema: “Ndio bila shaka. Najua kile ambacho tunataka kukifanya.

Nafikiri mtu aina hii, wakati wote anataka kufanya ligi yetu (Ligi Kuu) kuwa bora kabisa.

“Walitufunga sisi pale Stamford Bridge – na dhidi ya Napoli tulifungwa pia msimu uliopita. Zilikuwa mechi kali. Wakati wa mechi zile wao walikuwa bora kuliko sisi. “Lakini watu kwa kweli hawajui jinsi ilivyo ngumu. Mara nyingi nimekuwa nasema, mwaka wangu wa kwanza ulikuwa mgumu pia. Wakati fulani tulicheza vizuri, lakini hatukuwa na mwendelezo. “Watu wanatarajia, kocha anapowasili, ananunua wachezaji na mara moja anapata matokeo, lakini ukweli anahitaji muda. Inategemea unavyoaminika kutoka kwa wamiliki, watu waliopo katika timu, wanatakiwa kuamini hilo.”

Soma pia:  Klopp: Liver haitatumia fedha nyingi kusajili

Kufuatia kipigo hicho cha mabao 6-0 kutoka kwa Man City, Sarri baada ya kumalizika kwa mchezo huo, alikwenda moja kwa moja katika njia ya kuendea katika vyumba vya kubadilishia nguo, akionekana kupuuza mkono wa Guardiola.

“Nilizungumza na kocha msaidizi (Gianfranco Zola),” aliongeza Guardiola. “Maurizio Sarri hakuniona. Nina uhusiano mzuri sana naye, hivyo hakuna tatuzo kabisa.”

Comments

Comments are closed.

More in Michezo