Michezo

Higuain matumaini yote kwa Sarri

0
Higuain matumaini yote kwa Sarri
Gonzalo Higuain

Gonzalo Higuain amesema kocha Maurizo Sarri atapata ubora wake kwenye klabu ya Chelsea kama ilivyokuwa akiwa na Napoli.

Higuain alijiunga na Chelsea kwa mkopo wa miezi sita wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari na kuonesha kiwango kwa kuifungia Chelsea mabao mawili kwenye ushindi wa timu hiyo wa mabao 5-0 dhidi ya Huddersfield.

Kwenye mahojiano na kituo cha Skysport, Higuain alisema anaamini Sarri atamrejesha kwenye makali yake katika Ligi Kuu ya England.

“Ni kocha aliyepata ubora wangu,” alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31. “Namjua vizuri na ananijua vizuri. “Nina imani nitarejea kwenye makali yangu, haya ni malengo yangu. Ni mtu fulani aliyenisaidia, anayejua soka langu na anajua kupata ubora wangu.

Soma pia:  Real Madrid yaanza vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya

“Nina furaha sana kuwa hapa. Ni klabu nzuri yenye uwanja mzuri, hakika ni uzoefu mzuri kuwa hapa. Nina imani kadiri ya muda timu itaweza kufanikisha malengo yake yote.”

Higuain alijiunga na Chelsea akitokea AC Milan baada ya kuwa na kipindi kibaya kwenye klabu hiyo ya Italia akiwa amefunga mabao manane kwenye mechi 22 alizocheza kwenye mashindano yote.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo