Michezo

Simba SC kuandaa bajeti ya Usajili

0
Simba SC kuandaa bajeti ya Usajili
Mo Dewji

Mabingwa wa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara wanaandaa bajeti kubwa kwa ajili ya kununua wachezaji wenye uwezo wa kushindana na kuacha utamaduni wa kuleta wachezaji kuja kufanya majaribio kwenye timu hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mwekezaji wa Simba Mohamed ‘Mo’ Dewji alipozungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu masuala mbalimbali ya klabu hiyo.

Alisema wanamuomba Mungu mambo yakae sawa watetee ubingwa wa Ligi Kuu Bara ili wapate fursa kuwakilisha tena kwenye michuano kimataifa mwakani.

“Mipango yetu ni kuandaa bajeti kubwa kununua wachezaji watakao kuja kushindana kuepuka utamaduni wa kuchukua wachezaji kuja kufanya majaribio,”alisema Mo.

Aidha, alisema, kwenye kikao chao cha Bodi walijadili suala la kutafuta Kocha Msaidizi na kwamba jukumu hilo amepewa CEO wa klabu hiyo Crescentius Magori.

Soma pia:  Mtibwa Sugar: Sasa ni zamu ya Simba

Aussems amekuwa anafanya kazi kwa muda mrefu sasa bila ya kuwa na msaidizi baada ya aliyekuwa msaidizi wake Masoud Djuma kufutwa kazi.

Inadaiwa kuwa tayari imeshawekwa orodha ya makocha wasaidizi ambao ni Juma Mgunda wa Coastal Union, Etiene Ndayiragije wa KMC, Suleiman Matola wa Lipuli na Amri Said wa Biashara.

“Sambamba tunahitaji kupata mkurugenzi wa ufundi watu wa saikolojia na idara nyingine za wataalamu wa mchezo wa mpira kuhakikisha shabaha yetu inatimia,” alisema.

“Malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo isipofanikiwa msimu huu itafanikiwa siku zijazo.” Alisema watahakikisha wanajenga miundombinu ikiwemo kuanzisha kituo cha vijana ili kuzalisha wachezaji watakaokuja kuisaidia timu ikiwemo ile ya wanawake Simba Queens.

Soma pia:  Arsenal yakaribia kumsajili Ceballos

Uwanja wa Simba

Miundombinu ya uwanja wao ulioko Bunju Dar es Salaam iko tayari kwa ajili ya kufanyia mazoezi kilichobaki ni kwenda kumalizana na Serikali ili wawapatie nyasi bandia uanze kutumika.

Nafasi za ajira

Alisema siku za hivi karibu watatangaza nafasi za kazi kwa wenye taaluma sehemu mbalimbali kwa wanaohitaji kufanya kazi na timu hiyo kwa kuwa wameshaingia kwenye mfumo wa kampuni.

“Kwa wanaohitaji kazi wanakaribishwa sana kuomba na watalipwa vizuri kwa kuitumikia Simba vizuri na usaili utafanyika ili kupata watu wenye weledi,” alisema.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo