Michezo

Simba yampa mkataba wa miaka miwili Kagere

0
Simba yampa mkataba wa miaka miwili Kagere
Meddie Kagere

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba jana wameinasa saini ya Straika wa Kimataifa wa Gor Mahia ya Kenya, Meddie Kagere, ambaye ametia saini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Kagere ambaye ni mzaliwa wa Uganda mwenye Uraia wa Rwanda, alingara kwenye mashindano ya Sportspesa na kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo akipachika wavuni mabao manne.

Ujio wa nyota huyo ndani ya simba ni kama wamewafanyia umafia wapinzani wao, Yanga kwa kuwa awali ndio walionyesha nia ya kumsajili huku akihitaji TZS millioni 180 kujiunga na kikosi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kaimu wa Simba, Salim absallah maarufu kama ‘Try Again’, alisema Kocha Msaidizi wa klabu hiyo ambaye alikuwa na kikosi hicho katika mashindano ya Sportspesa yaliyofanyika Kenya, Masoud Djuma, aliomba saini ya nyota huyo ili kuongeza nguvu kwenye timu yake.

Soma pia:  Kauli ya Okwi kwa Simba, Okwi Kujiunga na Fujairah FC

“Tumetimiza alichokitaka kocha, kwa kuwa alitambua uwezo wa mchezaji na kaona ataongeza nguvu kwenye kikosi chetu, tumeamua kumletea alichokihitaji,” alisema Try Again.

Usajili wa Kegere ndani ya timu ya Simba unakuwa wanne baada ya kutanguliwa na nyota wengine watatu ambao walisajiliwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Nyota waliojiunga na Simba na timu walizotoka kwenye mabano ni Mohammed Rashid (Prisons), Adam Salamba (Lipuli FC) na MArcel Kaheza (Majimaji FC).

Ndani ya kikosi cha Simba ambacho kinafanya mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wapo nyota wengine wawili ambao ni raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa na Mnigeria Victor Patrick.

Wawa amerejea nchini mara ya pili ambapo awali alitua Azam FC mwaka 2014 kwa mkataba wa miaka miwili, baadae aliongezewa mwaka mmoja kabla ya kurejea na timu yake ya zamani ya El Merreikh ya Sudan alipomalizia mkataba.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo