Top Stories

TANROADS Kilimanjaro yalia na Madereva

0
TANROADS Kilimanjaro yalia na Madereva
Mkoani Kilimanjaro

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Kilimanjaro, wamelalamikia tabia zinazfanywa na baadhi ya madereva na matingo za kuharibu alama za Barabarani kwa kuzivunja kwa makusudi na zingine kuzifuta.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa TANROADS mkoani Kilimanjaro, Mhandisi Ntije Nkolante, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Alisema vitendo visivyo vya kiungwana vimekuwa vikigharimu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na serikali kuzirudishia alama hizo.

Mhandisi Nkolante alisema madereva hao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo kwa makusudi, bila kujali kuwa alama hizo zimekuwa zikiwasaidia katika kupunguza ajali za barabarani.

“Tulikuwa na tatizo la kuibwa kwa alama za barabarani na wananchi wasio na uzalendo na kuziuza kama vyuma chakavu, lakini baada ya kuona tatizo hilo, tuliamua kubadilisha na kuweka alama zenye nguzo za zage lakini tatizo lilioibuka sasa ni madereva kuzivunja alama hizo kwa makusudi,” alisema.

Soma pia:  Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara

Alisema alama ambazo wamekuwa wakishindwa kuzivunja wamekuwa wakizifuta, huku wakitambua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na inaweza kuchangia ajali na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia.

Meneja huyo alisema kwa mujibu wa uchunguzi watumiaji wa barabara ambao ni madereva wa Malori na Mabasi ya abiria wamekuwa mstari wa mbele kuharibu alama hizo.

Kwa mujibu wa Mhandisi Nkolante, barabara hizo siyo kwajili ya Chama wa Wamiliki wa Mabasi wa Mabasi (TABOA) pekee.

“Madereva wa malori na mabasi wamekuwa wakifanya makusudi kuvunja na kuziharibu alama za barabarani, wao wanazifahamu vizuri barabara hizo kwani wanapita kila kuchwao bila kutambua kuwa wapo wageni ambao hawazijui vizuri hizo, hivyo wanahitaji msaada wa vibao vya lama za barabarani,” alisema.

Soma pia:  Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara

Akizungumzia hali ya uharibifu wa barabara unaotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, Meneja huyo alisema hadi sasa hakuna uharibifu uliotokea na barabara zote ni salama.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories