Michezo

Michael Wambura aingangania TFF

0
Wambura aingangania TFF
Michael Wambura

Wakati kamati ya rufaa ya Shirikisho la soka Tanzana (TFF), juzi imetupilia mbali rufani ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo.

Michael Richard Wambura aliyepinga kufungiwa maisha, Wambura jana amesema atasonga mbele kudai haki yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Wambura alisema kuwa ataendelea kudai haki yake hadi mwisho.

Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani, Ebenezer Mshana, ametoa uamuzi ambao alikuwa anafahamu wazi kuwa watatoa maamuzi kama hayo kutokana na mazingira yaliyopo.

“Nimeshangaa kuona jana kwenye hukumu wakaona waongezee vitu vipya ambavyo havikuwepo kwenye Kamati ya Maasili kama suala la mimi na Simba lilingiaje pale wakati mimi na Simba tayari kesi iliisha,”

“Kama hawaamini waende pale Mahakama ya Kisutu wakathibitishe ila kiukweli mimi sijakubaliana ana maamuzi hayo na sasa nakata rufani tena na nipo tayari kufika mbali zaidi ili niweze kupata haki yangu.” alisema Wambura

Kauli hizo, zimekuja siku mbili baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ebenezer Mshana kutoa hukumu dhidi ya Wambura.

Alisema jana kwenye Makao Makuu ya TFF yaliyopo Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam  wakati akizungumza na vyombo vya habari. Alisema wamepitia malalamiko na vielelezo vyote kupitia kwa mawakili na kugundua Wambura ametenda kosa.

Ebenezer Mshana alisema adhabu aliyopewa kiongozi huyo si sahihi kutokana na ukubwa wa kosa kufuatia cheo alichokuwa nacho.

“Adhabu hiyo iendelee na ninapendekeza wapeleke kwenye vyombo husika ili hatua za kisheria ziweze kufuata”. alisema Mshana.

Aliongeza kuwa hiyo itakuwa fundisho kwa viongozi wengine kufanya makosa kama hayo.

Uamuzi huo, umekuja baada ya Kamati ya Maadili ya TFF mwezi uliopita kumfungia kiongozi huyo kwa mujibu wa kifungu cha 73 (1) (c) cha kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013.

Baada ya kupatikana na kosa la kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali, kudaiwa kugushi barua na kushusha hadhi Shirikisho.

Ni baada ya TFFkukopa mkopo wa Dola za Marekani 30,000 bila ya kufuata taratibu zozote zilizopo.

Pia Kamati hiyo ya Maadili ya TFF, nayo ilifikia vifungu mbalimbali vya kanuni za maadili ya TFF na kuridhika kusipokuwa na shaka.

Kamati hiyo, imemfungia Michael Wambura kifongo cha kutojihusisha na mpira wa miguu maisha.

Adhabu hiyo imetolewa kulingana na uzito wa kesi yake kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013″.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo