Michezo

Mtibwa Sugar: Sasa ni zamu ya Simba

0
Mtibwa Sugar na Simba
Thobias Kifaru

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar, umeeleza kwamba baada ya kuifunga Singida United sasa ni zamu ya Simba kuisambaratisha.

Akizungumza jana kutoka Mkoani Singida, Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru alisema wana imani “Mnyama lazima afe’.

“Kifo cha Simba kipo Morogoro hawatoki tutawapa kipigo kitakatifu”, alisema Thobias Kifaru.

Mtibwa Sugar iliweza kuichapa Ijumaa iliyopita timu ya Singida Unite kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Namfua.

Simba S.C
Simba S.C

Hata hivyo, Thobias Kifaru amekiri wanakwenda kucheza na Simba katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro hapo kesho kwa umakini mkubwa.

Soma pia:  Mambo yaiva Simba vs Al Ahly Taifa kesho

Comments

Comments are closed.

More in Michezo