Michezo

Ngassa aitabiria Simba Ubingwa

0
Simba Ubingwa
Simba

Winga wa zamani wa Simba na Yanga, Mrisho Ngassa amesema kuwa msimu huu Wekundu wa Msimbazi watakuwa Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Ngassa ambaye kwa sasa anachezea Ndanda FC ya Mtwara alisema  kama Simba watakaza zaidi kusaka ushindi lazima ubingwa uenda Msimbazi.

Mrisho Ngassa
Mrisho Ngassa

Alisema kuwa Simba wapo vizuri sana kutokana na kuundwa na kikosi imara zaidi.

“Kwa sasa kuna tofauti kubwa ya wachezaji ukulinganisha na miaka mingine iliyopita, kwahiyo kama watakomaa kusaka ushindi, wanaweza kutwaa Ubingwa,” alisema Mwisho Ngassa.

Hata hivyo, Ngassa alionya kuwa endapo watazubaa kidogo, wanaweza kujikuta wakijiharibia mipango yao, kwani kasi ya wapinzani wao Yanga na Azam si mchezo.

Soma pia:  Kauli ya Okwi kwa Simba, Okwi Kujiunga na Fujairah FC

Comments

Comments are closed.

More in Michezo